Assad asisitiza hatajiuzulu
Rais wa Syria Bashar al Assad amesisitiza kuwa hatajiuzulu kabla ya mwisho wa kipindi chake madaraka mwaka 2014, wakati bomu lililotegwa katika gari liua watu watatu katika mji mkuu Damascus.
View ArticleMakabiliano makali yaendelea Qusayr, Syria
Wapiganaji 30 wa kundi la wanamgambo la Hezbollah wanaripotiwa kuuwawa katika mapigano yaliyotokea katika mji wa Qusayr nchini Syria huku wengine zaidi ya 70 wakijeruhiwa.
View ArticleWaziri mkuu mpya wa China Li Keqiang ziarani India
Waziri mkuu mpya wa china Li Keqiang ameichagua India kuwa kituo cha kwanza cha ziara yake nchi za nje na kuahidi kurejesha hali ya kuaminiana kati ya Beijing na New-Delhi.
View ArticleSchalke wakamata nne, Düsseldorf watimuliwa
Ilikuwa siku ya mwisho yenye kizaazaa katika msimu wa kuadhimisha mwaka wa 50 wa Bundesliga wakati vita vya kucheza Ulaya na vita vya kupambana kuepuka kushushwa daraja vikiamuliwa
View ArticleKimbunga chaua 91 Oklahoma
Kimbunga kikubwa kilichoukumba mji wa Oklahoma nchini Marekani kimeuwa watu 91 wakiwemo watoto 20. Maafa makubwa yametokea katika kitongoji cha Moore, ambacho kimepitiwa na upepo unaosafiri kwa kasi ya...
View ArticleVita vya dola na vyombo vya habari nchini Uganda
Polisi nchini Uganda bado wamezingira kwa siku ya pili ofisi za baadhi ya vyombo vya habari vikuu nchini Uganda.
View ArticleSyria na Kasheshe ya ndege bila ya rubani magazetini
Hali nchini Syria,kishindo cha ndege inayorushwa bila ya rubani na kashfa ya kupendeleana katika chama cha CSU ni miongoni mwa mada zilizogonga vichwa vya habari vya magazeti ya Ujerumani.
View ArticleObama kuizuru Afrika, Kenya haimo katika ratiba
Rais Barack Obama wa Marekani anatarajiwa kufanya ziara barani Afrika mwezi ujao, ambayo itamfikisha katika nchi za Senegal, Afrika Kusini na Tanzania, lakini nchi yake ya asili Kenya haimo katika ratiba.
View ArticleMabaki ya Silaha za Libya bado ni tishio katika ukanda huo.
Umoja wa mataifa umesema vikosi vyenye silaha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati,vinatumia silaha ambazo zinadhaniwa ni mabaki ya silahi zilizotumika Libya mwaka 2011,kuuwa tembo kwa ajili ya biashara ya...
View ArticleSekta ya mafuta Uganda kwenye kashfa nzito
Hata kabla ya uchimbaji wa mafuta kuanza, sekta ya mafuta nchini Uganda imekumbwa na madai ya hongo dhidi ya maafisa wa serikali, kesi zinazohusiana na kodi nje ya nchi, ambazo zinaigharimu serikali...
View ArticleBan Ki-moon aanza ziara Maziwa Makuu
Benki Kuu ya Dunia itatoa dola bilioni 1 kusaidia maendeleo ya eneo la maziwa makuu. Rais wa Benki hiyo Jim Yong Kim ameyasema hayo mjini Kinshasa alikowasili akiandamana na katibu mkuu wa Umoja wa...
View ArticleRipoti ya Tume ya Maridhiano yawataja Kenyatta, Ruto
Viongozi wa ngazi za juu nchini Kenya, wakiwemo Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto, ni miongoni mwa waliopendekezwa kushtakiwa katika ripoti ya kushtusha iliyotolewa na Tume ya TJRC.
View ArticleShambulio la kigaidi London
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron leo ameitisha kikao cha dharura na wakuu wa kijasusi na kiusalama baada ya washambuliaji wawili kumuua mwanajeshi mmoja kwa kumkata kata kwa mapanga mjini London..
View ArticleMiaka 150 ya chama cha SPD
Chama cha Kisoshalisti cha Ujerumani, SPD, Alhamisi kimesherehekea miaka 150 ya kuanzishwa kwake, huku Kansela Angela Merkel akitoa sifa kwa wapinzani wake hao, kwa kuwaita sauti ya demokrasia...
View ArticleOmbi la Kenya kuhusu ICC lakataliwa na Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelikataa ombi la Kenya la kutaka kufutiliwa mbali kwa kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto katika mahakama ya ICC kutokana na ghasia za...
View ArticleMuseveni ambadilisha mkuu wa majeshi kuwa waziri wa mambo ya ndani
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amefanya mabadiliko ya ghafla katika safu za uongozi serikalini na jeshini kwa kumuondoa mkuu wa majeshi, Aronda Nyakairima, na kumpa nafasi ya uwaziri wa mambo ya ndani.
View ArticleMtwara bado hali tete
Hali mkoani Mtwara, kusini ya Tanzania, inaendelea kuwa ya wasiwasi kufuatia ghasia za hapo majuzi kupinga uamuzi wa serikali kutaka kujenga bomba la kusafirisha gesi kutoka eneo hilo kuelekea Dar es...
View ArticleUmoja wa Afrika watimiza nusu karne
Umoja wa Afrika unatimiza miaka 50 tangu kuundwa kwake hapo tarehe 25 Mei 1963 kwa jina la Umoja wa Nchi Huru za Afrika kuongoza mapambano dhidi ya ukoloni na kumaliza utawala wa ubaguzi wa rangi...
View ArticleGoma,Nigeria na Afrika kusini magazetini wiki hii
Mapigano Goma,kuzingirwa na jeshi,ngome ya wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam wa Nigeria- Maiduguri na mvutano kuhusu haki miliki ya jina la rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini Nelson...
View ArticleWembley yawakaribisha Dortmund na Bayern
Makao ya soka ya Uingereza yanaukaribisha mngurumo wa sauti za Wajerumani Jumamosi wakati Bayern Munich wakikwaruzana na Borussia Dortmund katika uga wa Wembley. Nani atalileta kombe Ujerumani?
View Article