Rais Saleh asaini makubaliano ya kuacha madaraka
Hatimaye Rais Ali Abdulla Saleh wa Yemen amesaini makubaliano yanayofungua njia ya kuondoka madarakani, akikabidhi madaraka hayo kwa makamo wake, naye akihakikishiwa kinga ya kutoshitakiwa.
View ArticleUmoja wa Mataifa waionya Ethipia kuhusu kupeleka majeshi Somalia
Umoja wa mataifa umeonya kuwa kitendo cha Ethiopia kupeleka vikosi vyake nchini Somalia kunaweza kuzorotesha zaidi hali mbaya ya usalama katika eneo hilo.
View ArticleHali nchini Misri-wanajeshi waomba radhi
Mapigano yamepamba moto kwa siku ya sita mfululizo mjini Cairo ambako maelfu ya waandamanaji wanadai jeshi liwakabidhi raia madaraka. Baraza kuu la kijeshi limeomba radhi kwa mauwaji ya raia.
View ArticleKamal Ganzouri atakiwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Misri
Imeripotiwa kwamba Baraza la Kijeshi la Misri limemteua Kamal al-Ganzouri kuwa waziri mkuu mpya lakini waandamanaji wanapinga na wanaendelea kukusanyika kwa maandamano dhidi ya utawala huo.
View ArticleWaandishi wa habari wanyanyaswa katika kipindi cha kampeni DRC
Kipindi cha kampeni ya uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kimeghubikwa na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya waandishi na vyombo vya utangazaji habari.
View ArticleSyria kutekeleza matakwa ya jumuiya za kiarabu au iwekewe vikwazo
Serikali ya Syria ina saa chache kukubali waangalizi wa kimataifa wakiwemo waandishi habari kuingia nchini humo na kuangalia mambo yanavokwenda la sivyo iwekewe vikwazo.
View ArticleBunge la Ujerumani lapitisha bajeti ya mwaka 2012
Wabunge wa Ujerumani wameridhia bajeti ya mwaka 2012, ambayo itakuwa na deni jipya la euro bilioni 26, ambalo ni kubwa kulinganisha na la mwaka 2011, lakini halihatarishi usalama wa kiuchumi wa taifa...
View ArticleYahya Jammeh atangazwa mshindi Gambia
Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, ameshinda muhula mwengine wa miaka mitano, baada ya Tume ya Uchaguzi kumtanganza mshindi wa uchaguzi wa Alhamis iliyopita.
View ArticleUchaguzi Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
Mikutano ya hadhara yapigwa marufuku mjini Kinshasa
View ArticlePakistan yaiamuru jumuiya ya NATO iondoke kambini
Shambulio la Jumamosi ni pigo kwa juhudi za Marekani kuimarisha ushirikiano na Pakistan katika kuvimaliza vita nchini Afghanistan
View ArticleGhasia siku ya mwisho ya kampeni DRC
Siku ya mwisho ya kipindi cha kampeni ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeghubikwa na ghasia baina ya mgombea mkuu wa upinzani Etienne Tshisekedi na polisi hapo jumamosi.
View ArticleUchaguzi mkuu wafanyika leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Uchaguzi wa leo unafuatia kampeni iliyogubikwa na machafuko ambapo watu wawili waliuwawa siku ya mwisho ya kampeni. Mji wa Lubumbashi ulikuwa kitovu cha machafuko kuelekea uchaguzi.
View ArticleWatu 23 wauwawa Syria huku jumuiya ya kiarabu ikiiwekea vikwazo
Raia wasiopungua 23 wameuwawa nchini Syria huku jumuiya ya nchi za kiarabu ikiiwekea vikwazo nchi hiyo. Uingereza imeipongeza hatua hiyo ikisema ni ishara kushindwa kwa utawala kutimiza ahadi zake...
View ArticleUpigaji kura waendelea DRC
Raia katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wanaendelea kumiminika vituoni kushiriki katika uchaguzi mkuu wa kuchagua rais, baada ya wagombea kufanya kampeni kali mjini Kinshasa iliokumbwa na vurugu.
View ArticleWamisri wamiminika vituoni kuchagua wabunge
Wamisri wapiga kura kulichagua bunge jipya katika uchaguzi uliosusiwa na baadhi waliokita kambi katika uwanja wa Tahrir.
View ArticleZoezi la kuhesabu kura , DRC laendelea
Zoezi la kuhesabu kura linaendelea katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo katika uchaguzi wa pili baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe,katika siku ya uchaguzi ambayo iligubikwa na hali ya mtafaruku na...
View ArticleDalili njema zaibuka kwenye mkutano wa Mazingira wa Durban
Wakati mazungumzo ya Jukwaa la Mataifa 194 juu ya Mabadiliko ya tabia nchi (UNFCC) yakiingia siku yake ya pili mjini Durban, kuna dalili ya hatua za kupunguza athari za gesi chafu kutoka sekta ya...
View ArticleMzozo wa madeni upatiwe ufumbuzi haraka
Rais wa Marekani Barack Obama ametoa mwito kwa viongozi wa Ulaya kuchukua hatua za dhati kuumaliza upesi, mzozo wa madeni unaohatarisha kanda nzima ya sarafu ya euro na hata ukuaji wa kiuchumi nchini...
View ArticleMgogoro wa Euro waleta serikali mpya Ulaya lakini siasa zile zile
Hadi hivi sasa, mzozo wa fedha ulioibuka mwaka 2007 kote duniani, umeshasababisha serikali mpya kuchaguliwa katika baadhi ya nchi za Ulaya - lakini ionekanavyo, sababu halisi za mzozo huo wa fedha bado...
View ArticleMatokeo ya kura DRC yaanza kubandikwa
Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi yameanza kubandikwa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura katika jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo, huku hali ya usalama ikitajwa kuwa shwari katika mji mkuu Kishansa.
View Article