Quantcast
Channel: DW Kiswahili
Browsing all 28146 articles
Browse latest View live
↧

Papa Benedikt XVI ashangiriwa Freiburg

Nchini Ujerumani, takriban vijana 30,000 wameshiriki katika misa ya jioni iliyosomwa na Papa Benedikt wa 16 katika mji wa Freiburg.

View Article


Wahanga wa janga la njaa wahitaji msaada zaidi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ametoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kutoa mchango zaidi wa fedha kuwasaidia wahanga wa janga la njaa katika Afrika ya Mashariki.

View Article


Rais Saleh aitisha uchaguzi wa mapema

Rais Saleh ametaka ufanyike uchaguzi wa mapema katika hatua ambayo huenda isiwaridhishe waandamanaji wanaomtaka aondoke madarakani.

View Article

Profesa Wangari Maathai afariki dunia

Maathai amefariki dunia jana jijini Nairobi baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu. Kifo chake ni pigo kubwa kwa wanaharakati wa mazingira na bila shaka kwa ulimwengu kwa ujumla.

View Article

Mahojiano na Mwanaharakati Hassan Omar Hassan kuhusu kifo cha Profesa Wangari...

Marehemu Profesa Wangari Maathai atakumbukwa kwa juhudi zake za kuyasukuma mbele masuala ya haki za binadamu na ulinzi wa mazingira.

View Article


Mrengo wa shoto wadhibiti baraza la Seneti Ufaransa

Vyama vya mrengo wa shoto vimefanikiwa kulidhibiti baraza la Seneti kutoka vyama vya mrengo wa kulia nchini Ufaransa kwa mara ya kwanza katika historia katika uchaguzi uliofanyika jana.

View Article

Hali ni tete nchini Yemen

Upande wa upinzani nchini Yemen umekula kiapo dhidi ya rais Ali Abdallah Saleh wanaedai hatekelezi ahadi anazotoa na hasemi lini atang'oka madarakani.

View Article

Wanajeshi wa baraza la mpito wateka bandari ya Sirte

Wanajeshi wa utawala mpya wa Libya wanaidhibiti bandari ya mji wa Sirte- ngome ya kiongozi wa zamani Muammar Gaddafi. Mamia ya watu wanaukimbia mji huo.

View Article


Guinea yakumbuka mauaji ya 2009

Leo (28.09.2011) ni miaka miwili kamili tangu jeshi la Guinea lilipowavamia waandamanaji katika uwnaja wa mpira mjini Conakry na kuwauawa zaidi ya 100 katika tukio linalotajwa kama mauaji ya maangamizi.

View Article


Ugiriki yatapatapa hatima ya mfuko wa uokozi kujadiliwa

Bunge la Ujerumani linajiandaa kulipigia kura suala la kuuongeza uwezo na kiwango cha mfuko wa fedha wa kuyanusuru mataifa yanayokabiliwa na madeni na nakisi za bajeti.

View Article

Wapiganaji dhidi ya Gaddafi wapata hasara kubwa Sirte

Vikosi vinavyompinga Muammar Gaddafi vimepata hasara kubwa leo wakati vikielekea kwenye eneo la kiongozi huyo wa Libya aliepinduliwa katika mji alikozaliwa wa Sirte na pia wamepata kipigo katika mji wa...

View Article

Libya yaahidi ushirikiano kuchunguza shambulio la Lockerbie

Watawala wapya wa Libya wamesema wako tayari kushirikiana watakapotakiwa kuwakabidhi watu wahojiwe kuhusiana na shambulio la bomu dhidi ya ndege ya abiria katika anga ya Lockerbie nchini Scotland mnamo...

View Article

Bundestag yaidhinisha mfuko wa uokozi wa Ulaya ulio madhubuti

Bunge la Ujerumani, Bundestag, limepiga kura na kuiamua hatima ya mfuko wa uokozi mahsusi kwa mataifa yanayokabiliana na madeni makubwa na nakisi ya bajeti.

View Article


Tanzania: Sakata la Dowans

Nchini Tanzania Mahakama Kuu ilitoa hukumu ya kuridhia malipo ya fidia ya fedha kwa Kampuni ya ya Dowans ambayo ilisajili,tuzo yake iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya...

View Article

Rais Sata aondolewa marufuku ya kuingia Malawi

Serikali ya Malawi imesema imeondosha marufuku ya kuingia nchini humo kwa rais mpya wa Zambia, Michael Sata, ikiwa ni kutatua mkwamo wa kibalozi kuelekea mkutano wa COMESA unaofanyika nchini Malawi...

View Article


Masoko yarudia kupata faida baada ya bunge la Ujerumani kupiga kura

Masoko ya hisa ya Ulaya na Marekani yamepanda tena baada ya bunge la Ujerumani kuunga mkono kwa kauli moja upanuzi wa mfuko wa eneo la mataifa ya euro wa uokozi pamoja na madaraka yake.

View Article

Mapambano yanaendelea Libya

Umoja wa mataifa na duru nyengine zimeripoti kuwa raia wanaukimbia mji uliozungukwa wa Sirte nchini Libya ambako mapigano ya kuwaondoa wafuasi wa Muammar Gaddafi, yamesababisha vifo vya watu wengi

View Article


Kiongozi wa al-Qaeda nchini Yemen al-Awlaki auwawa

Mhubiri wa dini ya Kiislamu mzaliwa wa Marekani na mtu maarufu katika kundi la al-Qaeda Anwar al-Awlaki , ameuwawa katika shambulio la anga la Marekani mashariki ya Yemen.

View Article

Mji wa Sirte bado umezingirwa

Mji wa Sirte nchini Libya, mahali alikozaliwa kiongozi aliyeondolewa madarakani Muammar Gaddafi unaendelea kuzingirwa na majeshi yanayounga mkono baraza la mpito la taifa.

View Article

Je Ugiriki itafanikiwa kupata mkopo mwingine?

Ugiriki itakosa kufikia malengo yake ya mwaka huu na ya mwaka ujao ya kupunguza nakisi kwenye bajeti yake

View Article
Browsing all 28146 articles
Browse latest View live