Wakulima wazungu nchini Zimbabwe mashakani
Wakulima wazungu wa Zimbabwe wanakabiliwa na vitisho vipya vya kufukuzwa kutoka mashamba yao. Wengi walipokonywa mashamba katika machafuko yaliyoanza mwaka 2000 na waliobakia sasa wameingiwa na wasiwasi.
View ArticleBundeswehr waruhusiwa kuwapatia mafunzo Peschmerga
Ujerumani inapanga kuitika wito wa wanamgambo wa kikurd Peshmerga na kutuma silaha zaidi na vipuri kaskazini ya Iraq mwezi ujao wa februari
View ArticleKundi lenye mafungamano na IS lafanya mashambulizi Misri
Idadi ya waliouawa katika mashambulizi yaliyowalenga wanajeshi na polisi katika rasi ya Sinai, Misri imeongezeka hadi 40 huku Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi akikatisha ziara nchini Ethiopia na...
View ArticleMazungumzo mapya ya amani ya Ukraine
Wapatanishi kutoka Ukraine, Urusi na Ulaya wanajiandaa kwa mazungumzo mapya ya amani katika juhudi za kukomesha mapambano kati ya serikali ya Ukraine na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.
View ArticleKombe la Afrika laingia awamu ya mtoano
Guinea yaingia robo fainali na inapimana nguvu na Ghana siku ya Jumapili, wakati wenyeji Guinea ya Ikweta ina miadi na Tunisia na Algeria itaoneshana kazi na Cote D'Ivoire katika fainali za kombe la...
View ArticleBayern Munich yabugizwa 4-1
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wameanza vibaya sehemu ya pili ya msimu baada ya mapumziko ya kipindi cha baridi, kwa kubugizwa magoli 4-1 na Wolfsburg iliyo katika nafasi ya 2, kwenye mechi pekee...
View ArticleRais wa zamani wa Ujerumani Weizsäcker afariki dunia
Rais wa zamani wa Ujerumani Richard Wizseäcker ambaye alikuwa akiheshimiwa kimataifa kama kiunganishi cha kuungana upya kwa Ujerumani amefariki dunia Berlin Jumamosi (31.01.2015) akiwa na umri wa miaka...
View ArticleCongo na Guinea ya Ikweta zatinga nusu fainali
Soka barani Afrika limepata kufikia hali ya juu ya kupendeza lakini pia liliingia doa Jumamosi(31.01.2015),kutokana na vitendo vya fujo pale mwamuzi aliposhambuliwa baada ya wenyeji Guinea ya Ikweta...
View ArticleDunia yalaani kuuwawa kwa kukatwa kichwa mwandishi Kenji Goto
Jumuiya ya kimataifa imelaani mauaji kwa kukatwa kichwa ya mwandishi wa habari wa Japani Kenji Goto yaliofanywa na kundi la Dola la Kiislamu IS ambapo Japani imeapa kuwafikisha wahusika mbele ya mkono...
View ArticleMahasimu wa Sudan Kusini wasaini makubaliano ya amani
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na kiongozi wa waasi, Riek Machar leo (02.02.2015) wamesaini makubaliano mapya ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya miezi 13.
View ArticleMapigano yapamba moto Ukraine
Mapigano makali yameripotiwa kati ya vikosi vya serikali na waasi wanaoiunga mkono Urusi wanaong'ang'ania udhibiti wa eneo muhimu la usafiri la Debaltseve.
View ArticleMaoni: Afrika yapiga hatua
Viongozi wa Umoja wa Afrika wamemaliza mkutano wao. Ludger Schadomsky wa DW anakosoa kuchaguliwa na mkongwe Robert Mugabe kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo lakini anasema pia mkutano umeleta mafanikio.
View ArticleGhana na Cote D'Ivoire zachukua nafasi zao halisi barani Afrika
Timu nne zimefanikiwa kuingia katika nusu fainali ya kombe la mataifa ya Afrika ,Cote D'Ivoie yaitoa timu bora, Algeria mashindanoni.
View ArticleWaziri Mkuu wa Ugiriki anaendelea na ziara yake Ulaya
Waziri Mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, anaendelea na ziara yake Ulaya, huku akiwa na matumaini ya kuungwa mkono na Italia katika jitihada zake za kuujadili upya mpango wa kuunusuru uchumi wa nchi yake.
View ArticleWilliam Schabas ajiuzulu wadhifa wake
Mkuu wa tume ya haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa inayochunguza mgogoro uliotokea kati ya Israel na Palestina William Schabas, amejiuzulu kufuatia madai ya upendeleo katika kazi yake yaliotolewa na...
View ArticleRais wa Ujerumani azuru Tanzania
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck yuko nchini Tanzania kwa ziara rasmi ya siku sita. Kiongozi huyo amepokewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.
View ArticleUN:Pande zote mzozo wa Ukraine zauwa raia
Umoja wa Mataifa umekosoa mbinu za kivita zinazotumiwa na pande zinazohasimiana nchini Ukraine, na kuzitaka pande hizo kuupa kipaumbele usalama wa raia.
View ArticleTatizo la huduma za afya mashariki mwa Ukraine
Watu waliotengwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kupata huduma msingi za afya katika eneo la Ukraine linalokabiliwa na vita. Eneo hilo liko katika hatari ya kutumbukia kwenye mzozo mkubwa wa...
View ArticleUmoja wa Ulaya kuiregezea kamba Ugiriki ?
Halmashauri ya Umoja wa Ulaya imeashiria kuwa tayari kuzifanyia marekebisho sera zake za kiuchumi lakini imegoma kufanya mabadiliko ya jumla ili kuifurahisha serikali ya nchi hiyo yenye kupinga sera ya...
View ArticleRais wa Ujerumani aendelea na ziara yake Tanzania
Rais Joachim Gauck wa Ujerumani anaendelea na ziara yake nchini Tanzania, ambapo jana alikula chakula cha jioni alichoandaliwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye ikulu ya Magogoni...
View Article