Nigeria,Jamhuri ya Afrika Kati na Pistorius magazetini
Kutekwa nyara wasichana zaidi ya 200 na Boko Haram ,mauwaji katika jamhuri ya Afrika kati na Oscar Pistorius kutakiwa akapime kama akili yake inafanya kazi ni miongoni mwa mada za bara la Afrika...
View ArticleBlatter: Ni "kosa" Qatar kuandaa Kombe la Dunia 2022
Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni – FIFA Sepp Blatter amesema ilikuwa kosa kuichagua Qatar kuandaa dimba la Kombe la Dunia mwaka wa 2022 kwa sababu ya hali ya joto kali nchini humo
View ArticleModi aahidi India mpya
Waziri Mkuu mteule wa India, Narendra Modi, ameahidi kutimiza ndoto za raia bilioni 1.2, huku chama tawala cha Congress kikiri kushindwa na viongozi kadhaa wa kimataifa wakimpongeza Modi kwa ushindi wa...
View ArticleWatu 10 wauwawa kwenye milipuko Nairobi, Kenya
Watu wengine zaidi ya 70 wamejeruhiwa katika milipuko miwili kwenye eneo la shuguli nyingi la soko, Nairobi. Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ametoa risala za rambirambi kwa familia za wahanga wa hujuma...
View ArticleMarekani kuizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia
Waziri wa mambo ya ndani wa Marekani Chuck Hagel amewaahidi viongozi wa Israel kwamba Marekani itafanya kile inacholazimika kufanya kuzuia Iran kuwa taifa lenye kumiliki silaha za nyuklia
View ArticleMarekani kuizuia Iran kumiliki silaha za nyuklia
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel amewaahidi viongozi wa Israel kwamba Marekani itafanya kile inacholazimika kufanya kuzuia Iran kuwa taifa lenye kumiliki silaha za nyuklia
View ArticleNarendra Modi, waziri mkuu mpya India
Kiongozi wa upinzani nchini India, Narendra Modi, atakuwa waziri mkuu mpya katika taifa hilo ambalo lina historia ndefu ya demokrasia, akishinda uchaguzi muhimu kuwahi kushuhudiwa katika nchi hiyo kwa...
View ArticleNigeria na majirani zake watangaza vita dhidi ya Boko Haram
Nigeria na majirani zake wameapa jana Jumamosi(17.05.2014) kuunganisha nguvu zao dhidi ya kundi la Boko Haram katika makubaliano yanayoelezwa kuwa ni tangazo la vita dhidi ya kundi hilo.
View ArticleChina yaondowa maelfu ya raia wake Vietnam
Vikosi vya usalama vimewekwa katika miji mikubwa Vietnam kuzima maandamano mapya yaliochochewa na utafiti wa kuchimba mafuta wa China katika eneo la bahari lenye mzozo wakati China ikiwaondoa maelfu ya...
View ArticlePapa ajutia mauaji ya wayahudi na wanazi
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewakumbuka wayahudi walioangamizwa katika mauaji ya Holocaust na mashambulizi ya kigaidi, katika siku ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu ya...
View ArticleWajumbe wa OSCE washikiliwa na waasi
Rais Mteule wa Ukraine Poroshenko amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais,wakati kiongozi wa waasi wa mashariki mwa Ukraine amesema wapiganaji wake wanawashikilia wajumbe wa OSCE
View ArticleVyombo ya habari nchini Kenya havina uzalendo?
Nchini Kenya waandishi habari wanadaiwa kutokuwa na uzalendo kwa namna wanavyoripoti juu ya masuala ya ugaidi yanayoendelea nchini humo.
View ArticleMatumizi ya nguvu yazidi makali Jamhuri ya Afrika Kati
Hali inatisha katika mji mkuu wa jamhuri ya Afrika Kati-Bangui ambako vizuwizi vimewekwa majiani na mapigano kuripotiwa kati ya vijana na vikosi vya polisi huku maelfu wakiandamana kudai serikali ya...
View ArticleAfrika yazidi kukua, lakini umaskini bado
Kwa ukuaji wa kiuchumi wa asilimia 5 kwa mwaka, bara la Afrika linaonekana kuepukana na madhara ya mtikisiko wa kiuchumi uliyoikumba dunia, lakini watalaamu wanaonya dhidi ya shauku iliyopitiliza.
View ArticleWaasi wadungua helikopta Ukraine
Rais Mteule wa Ukraine Petro Poroshenko ameapa kuwaadhibu waasi wanaoiunga mkono Urusi ambao wameiangusha helikopta ya kijeshi mashariki mwa nchi hiyo na kuuwa wanajeshi 12 akiwemo generali mmoja.
View ArticleMashambulizi dhidi ya waasi kuendelea Ukraine
Ukraine inadai kwamba imeyakombowa maeneo mengi yaliokuwa yakishikiliwa na waasi mashariki mwa nchi wakati serikali ya Marekani ikielezea wasi wasi wake juu ya kuonekana kwa wapiganaji kutoka Chechnya...
View ArticleAfrika katika magazeti ya Ujerumani
Wiki hii magazeti ya Ujerumani yanauzingatia ushindi wa Jenerali Abdel Fattah al-Sisi katika uchaguzi wa nchini Misri. Pia yameandika juu ya Boko Haram na biashara ya Uran baina ya Ufaransa na Niger
View ArticleMatumaini katika kambi ya kocha Löw
Dimba la Kombe la Dunia linang'oa nanga katika kipindi cha wiki mbili zijazo, na baada ya wiki iliyojaa misukosuko, hatimaye kuna habari nzuri kwa kikosi cha Ujerumani chake kocha Joachim Löw
View ArticlePeter Mutharika: Kutoka mshtakiwa wa uhaini hadi rais
Peter Mutharika, ambaye alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa Malawi siku ya Ijumaa, anajiandaa kuchukuwa hatamu ya uongozi wa taifa hilo maskini la kusini mwa Afrika chini ya kivuli cha mashtaka ya uhaini.
View ArticlePolisi wafyatua mabomu ya kutoa machozi Uturuki
Polisi nchini Uturuki wamefyatua mabomu ya kutoa machozi jana Jumamosi(31.05.2014)wakiwatawanya waandamanaji katikati ya mji wa Istanbul wakati wa kumbukumbu ya mwaka mmoja ya maandamano makubwa...
View Article