Quantcast
Channel: DW Kiswahili
Browsing all 28146 articles
Browse latest View live
↧

Pillay alikosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Mkuu wa Tume ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay amelikosoa vikali Baraza la Usalama la umoja huo kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti za kumaliza au hata kuzuia mizozo inayoendelea.

View Article


Marekani kuendelea na mashambulizi Iraq

Marekani imeonya kuwa vita dhidi ya waasi wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu huenda vikachukua muda mrefu sana. Wizara ya ulinzi ya Marekani imeliita kundi hilo tishio kubwa ambalo halijawahi kutokea.

View Article


Watu 15 wauwawa Ukanda wa Gaza

Hali bado imeendelea kuwa mbaya Ukanda wa Gaza. Taarifa kutoka huko zinaeleza watu 15 wamuwawa katika matukio mawili tofauti.

View Article

Milango ya msimu mpya wa Bundesliga yafunguliwa

Msimu mpya wa Bundesliga umeng'oa nanga. Lakini mafanikio ya Ujerumani katika Kombe la Dunia yana maana gani katika kandanda la Bundesliga? Jee, Bundesliga iko tayari kumenyana tena kimataifa?

View Article

Super Mario akaribishwa tena Uingereza

Soka la Uingereza linamkaribisha tena mmoja wa wachezaji wenye utata kabisa. Liverpool ilimuuza mchezaji Luis Suarez na sasa wamemnunua Mario Balotelli ili kulijaza pengo la mashambulizi

View Article


Afrika katika magazeti ya Ujerumani

Wiki hii magazeti karibu yote ya Ujerumani yameandika juu ya maradhi ya Ebola yaliyoripuka tena barani Afrika. Magazeti hayo pia yameandika juu ya vita vya kiwakala vinavyoongozwa na makanisa ya...

View Article

Ligi ya mabingwa wa dunia yaanza rasmi Bayern kidedea

Msimu wa ligi ya mabingwa wa dunia Bundesliga umeanza rasmi jana,(22.08.2014) na kama ilivyotarajiwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo , Bayern Munich wamefanikiwa kuibwaga VFL Wolfsburg kwa mabao 2-1.

View Article

Merkel na Obama walaani kitendo cha Urusi

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na Rais Barack Obama wa Marekani wameonya kuhusu hatari ya kuongezeka kwa mzozo wa Ukraine, baada ya Urusi kupeleka msafara wake wa malori mashariki mwa Ukraine.

View Article


Merkel ataka usitishaji mapigano Ukraine

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema Jumamosi (23.08.2014) mzozo wa Ukraine unaweza kutatuliwa lakini iwapo tu udhibiti utaimarishwa kwenye mipaka ya Ukraine na Urusi.

View Article


Hali ya wasi wasi yaongezeka Iraq

Mashambulio ya mabomu mjini Baghdad na mji wa kaskazini wa Kirkuk yamesababisha vifo vya takriban watu 42 nchini Iraq Jumamosi(24.08.2014) wakati serikali inachunguza shambulio baya kabisa dhidi ya...

View Article

Boko Haram yatangaza utawala wa Kiislamu

Kiongozi wa Boko Haram ameanzisha utawala wa Kiislam katika mji wa kaskazini mashariki mwa Nigeria uliotekwa na waasi mapema mwezi huu wakati ikiripotiwa polisi 35 wa Nigeria hawajulikani walipo.

View Article

Atletico Madrid walipiza kisasi dhidi ya Real Madrid

Atletico Madrid ya Uhispania imepata kiasi kunusa ulipizaji kisasi kutokana na kushindwa katika fainali ya Champions League msimu uliopita dhidi ya Real Madrid. Hivyo wajipiga kifua mjini Madrid

View Article

IS yaiteka kambi ya jeshi la anga Syria

Kundi linalojiita Dola la Kiislamu-IS limeikamata kambi muhimu ya jeshi la Syria ambayo ilikuwa ngome ya mwisho ya jeshi hilo katika jimbo la al-Raqqa. Naye mwandishi wa habari wa Marekani aliyetekwa...

View Article


Serikali ya Ufaransa yajiuzulu

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls, ametangaza kwamba serikali ya nchi hiyo inajiuzulu. Baraza jipya la mawaziri inatarajiwa kutangazwa Jumanne (26.08.2014). Hatua hii ni pigo kwa rais Francois...

View Article

Serikali na Renamo waafikiana Msumbiji

Serikali ya Msumbiji na kundi la waasi la Renamo chama kikuu cha upinzani, wametia saini makubaliano ya kumaliza vita vyao vya takriban miaka miwili.

View Article


Utata sera ya silaha ya Ujerumani

Wahariri wanahoji ikiwa sera ya Ujerumani ya silaha kuelekea maeneo yenye migogoro inakiukwa katika wakati ambapo Umoja wa Ulaya umeyaruhusu mataifa wanachama kulisaidia jeshi la Pashmerga, Iraq.

View Article

Kongo yathibitisha vifo kutokana na Ebola

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuweko na ugonjwa wa Ebola kwenye jimbo la Equateur. Waziri wa afya amesema kwamba watu 2 miongoni mwa 13 waliofariki wiki iliyopita wamekutwa na...

View Article


Dortmund, Schalke zaanza msimu kwa kichapo

Goli la haraka kuliko yote yaliyowahi kufungwa katika sekunde za mwanzo za mchezo yamezamisha makamu Borussia Dortmund katika mchezo wao wa kwanza katika msimu mpya Bundesliga

View Article

Wanajeshi wa Nigeria wakimbilia Cameroon

Kundi la Boko Haram hapo jana limeuvamia mji mmoja wa mpakani kaskazini mashariki mwa Nigeria, na kuwalazimu wakaazi na wanajeshi kutoroka na kuingia katika nchi jirani ya Cameroon wakiwemo wanajeshi

View Article

UAE yashambulia wanamgambo Libya

Maafisa wa Marekani wamsema ndege za kivita za Umoja wa Falme za Kiarabu zimefanya mashambulizi ya siri ambayo hayakutarajiwa kuyalenga maeneo ya wanamgambo wa Kiislamu nchini Libya.

View Article
Browsing all 28146 articles
Browse latest View live